Friday, April 17, 2020

NEWS: SIKU TATU ZA KULIOMBEA TAIFA

Hapo jana tarehe 16 April 2020, Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter akiwaomba watanzania wote kwa umoja wao kila mtu kwa Imani yake amuombe MWENYEZI MUNGU MUWEZA WA YOTE atuepushe na janga hili la corona.
"Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia." Alisema Mh. Rais John Magufuli.

 Tufuate taratibu zote za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona . "Tukijinge dhidi ya corona, Tuwalinde tuwapendao".


No comments: