Tuesday, December 26, 2017

ÑEW! NEW! NEW! NEW! KWA ADVANCE SOMA UJUE VITU

Imeletwa na ©MABULAMEDIA
Mtihani wa kidato cha sita (ACSEE)

Mtihani huu unafanywa na watahiniwa waliosoma miaka miwili ya sekondari ya juu (kidato cha tano na sita) na lazima wawe walifaulu masomo matatu ya kidato cha nne katika kiwango cha C.

Kalenda ya mtihani

Mtihani wa kidato cha sita hufanyika katika wiki ya kwanza ya mwezi mei ya kila mwaka.

Malengo ya mtihani wa kidato cha sita

Malengo ya mtihani huu ni kupima maarifa na uwezo wa wanafunzi wa kuendelea na elimu zaidi kama vile Stashahada na kozi za digrii; kuchunguza kiwango ambacho wanafunzi wanaweza kutumia stadi walizopata kupambana na changamoto za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hivyo, watahiniwa katika kiwango hiki wanatarajiwa kuwa na stadi zifuatazo katika shughuli mbalimbali: maarifa, ufahamu, matumizi, uchanganuzi, usanisi na tathmini.

Watahiniwa ambao Wanastahili Kufanya Mtihani

Mtihani huu unafanywa na watahiniwa waliomaliza miaka miwili ya elimu ya juu ya sekondari (ACSEE) na lazima wawe wamefaulu kwa kiwango cha C katika mosomo matatu ya kidato cha nne.

Masomo yanayotahiniwa

Masomo yanayotahiniwa katika Cheti cha Elimu ya Juu Sekondari ni kama yafuatayo: Stadi za Jumla ambalo ni somo la lazima; masomo mengine yamepangwa katika makundi kwa mchanganyiko, yaani sayansi asili ambayo ni pamoja na Fizikia, Kemia na Hisabati (PCM), Fizikia, Kemia na Biolojia (PCB), Fizikia, Jiografia na Hisabati (PGM), Uchumi, Jiografia na Hisabati (EGM), Kemia, Biolojia na Jiografia (CBG), Kemia, Biolojia na Kilimo (CBA) na Kemia, Biolojia na Chakula na Lishe ya Binadamu (CBN). Kategoria nyingine ni Mchanganyiko wa Sanaa ambao unajumuisha Historia, Jiografia na Lugha ya Kiingereza (HGL), Historia, Jiografia na Kiswahili (HGK), Historia, Kiswahili na Lugha ya Kiingereza (HKL), Kiswahili, Lugha ya Kiingereza na Kifaransa (KLF), Uchumi, Biashara na Utunzaji wa Hesabu (ECA) na Historia, Jiografia na Uchumi (HGE).

Miundo ya Mitihani

Kila somo lina muundo wa mtihani, ambao unafafanua mpangilio wa karatasi ya mtihani, utaratibu na maudhui ambayo mtihani huo unayabeba. Maelezo ya masomo yanayoshughulikiwa yameoneshwa katika miundo ya mitihani husika ambayo inaweza kupatikana katika kiungo cha miundo ya mitihani.

No comments: